Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Ndugu Othman Masoud Othman leo Februari 10, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza.
Ujumbe huo ulioongozwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Marianne Young, uliowajumuisha pia Bw. Jack Fenwick, Katibu wa Pili (Second Secretary) na Bw. Calum Stewart, ambaye ni Mkuu wa Desk la Tanzania (Desk Officer), umefika huko nyumbani kwake Chukwani, nje kidogo ya mji wa Unguja.
Mazungumzo kati ya Ndugu Othman na Balozi Young na ujumbe wake yalijikita kwenye masuala ya demokrasia na mwenendo wa hali ya kisiasa Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa
Februari 10, 2026.



0 Comments