Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27, ambapo katika kipindi hicho, inatarajia kukusanya nakutumia shilingi trilioni 62.334 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, maendeleo na kulipia deni la Taifa.
Mhe. Balozi Omar amesema hayo wakati akiwasilisha Mpango huo ambapo amesema kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 10.3 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2025/26.
Tukio hilo limeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa pia na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, (Mb), akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 kwenye Kamati ya Bunge zima, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 62.334. kwa mwaka 2026/27, sawa na ongezeko la asilimia 10.3.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, wakifuatilia uwasilishaji wa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Mbungeni jijini Dodoma.
Mawaziri, Wabunge na Viongozi wengine wakiwa katika Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Mbungeni jijini Dodoma ambapo yamewasilishwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. Tausi Kida, baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, bungeni jijini Dodoma.

.jpg)



.jpg)
.jpg)
0 Comments