6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA KATAVI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Deogratias Banuba, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo iliyopo Mpanda Mjini mkoani Katavi, Machi 16, 2026.

Muonekano wa jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi pamoja na Wing B katika mradi wa ujenzi unaoendelea Mpanda Mjini. Mradi wa shilingi bilioni 3 umefikia asilimia 59 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika Desemba 2026, ukiimarisha huduma bora za afya kwa wananchi wa Katavi na maeneo ya jirani.
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu  Nchemba akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Katavi.
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba  akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo, Mpanda Mjini, Machi 16, 2026.



















WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Post a Comment

0 Comments