Habari za Punde

DADI AWAKALIA KOONI MASHEHA

Na Yussuf Hamad, Pemba

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi amepiga marufuku utoaji vibali vya aina yoyote vinavyotolewa na Masheha wa mkoa huo ambavyo huhalalisha mauzo ya mashamba, viwanja na mifugo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini kuepo baadhi ya Masheha wanaotoa vibali kinyume na utaratibu na kusababisha kukosekana kwa mapato ya serikali.

Dadi alitoa agizo hilo alipofanya mazungumzo na Makamanda wavikosi vya usalama, Masheha na Watendaji wakuu wa mkoa huo, afisini kwake Wete.

'Nyinyi Masheha ni sehemu ya Serikali kuu kazi yenu ni kusimamia sheria, kanuni na taratibu za nchi na sio kutoa vibali vya mauziano ya bidhaa au mashamba', alisema.

Alisititiza kuwa kumpatia mtu kibali chochote bila ya kutolewarisiti ya Halimashauri ya wilaya au Baraza la Mji ni kosa kisheria kwani utakuwa umeikosesh serikali mapato ya asilimia 10.

Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa amepiga marufuku uingizaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki na kutoa wiki tatu kuangamizwa mifuko iliyoko katika maduka ya wafanyabiashara.

Amesema mifuko ya plastiki imekuwa ikiendelea kutumika ndani ya mkoa huo licha ya serikali kuzuia uingizaji na usambazaji wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.