Habari za Punde

NYONGEZA ZA WAFANYAKAZI ZILIZOSITISHWA KUREJESHWA

SERIKALI itawarejeshea nyongeza za mishahara watumishi wake baada ya kusitishwa tangu mwaka 2007.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir ameliambia baraza la Wawakilishi mjini hapa jana.

Waziri huyo alieleza hayo jana Barazani wakati akijibu swali la msingi la Mwakilishi Ali Salum Haji (Kwahani).

Mwakilishi huyo alitaka kujua, sababu gani zilizopelekea nyongeza ya mishahara ya kila mwaka kusitishwa tokea mwaka 2007.

Waziri huyo alisema serikali itarejesha nyongeza hizo pamoja na maslahi mengine yakiwemo mfumo mpya wa mishahara ndani ya mwaka wa fedha 2011/2012.

Kheir alisema nyongeza hizo zilsitishwa mwaka 2007, baada ya kurekebisha maslahi ya wafanyakazi kwa kuzingatia taaluma na viwango vya elimu vya wafanyakazi.

Alisema katika zoezi hilo la mwaka 2007, matatizo kadhaa yalijitokeza na ilibidi yafanyakazi wafanyiwe marekebisho kabla ya zoezi la kurejesha nyongeza hizo kuanza tena.

Aliyataja matatizo yaliyojitokeza na kupatiwa ufumbuzi ni pamoja na kuhakiki upya idadi ya wafanyakazi, kuangalia usahihi wa kumbukumbu za kielimu, kuweka muundo mpya wa mishahara na ngazi zake.

Aidha, waziri huyo alisema serikali ya awamu ya saba imedhamiria kwa dhati kuboresha maslahi ya watumishi wake ili waweze kumudu hali maisha

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.