Habari za Punde

DK SHEIN AMTEUA JAJI OMAR MAKUNGU KUWA KAIMU JAJI MKUU WA ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akimwapisha Jaji Omar Othman Makungu kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar leo.

Karibuni Jaji Makungu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Rais na kuapishwa kwa mujibu wa taratibu za kiutawala ambapo kuwa Kaimu Jaji Mkuu ni lazima uapishwe tena na Rais. 

Kwa hivyo usije ukaingiwa na dukuduku kwamba tayari huyu amekwishaapishwa kama ni Jaji wa Mahkama Kuu hivyo kuna haja gani kuapishwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu? Ni kwa mujibu wa taratibu hivyi ni vyeo na dhamana tofauti ambazo zote kisheria ni lazima kuapishwa.

Ila kitu kimoja kinachoshangaza ni kwamba kabla ya kuteuliwa Jaji wa Mahkama Kuu, ndugu Makungu alikuwa akijulikana kama ni Jaji kwani  aliwahi kuwa Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, nafasi ambayo hupewa mtu mwenye cheo cha Ujaji na si vyenginevyo.

Wakati huo alikuwa ni Jaji wa Mahkama gani mpaka ikabidi ateuliwe tena kuwa Jaji wa Mahkama Kuu? Jibu nililo nalo ni kwamba labda pale alipoteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu alipoteza sifa ya Ujaji na ndiyo maana ikambidi ateuliwe tena. Wajuzi wa Sheria tupeni ufafanuzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.