Na Suleiman Rashid, Pemba
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Said Ali Mbarouk ameitaka kamati ya soko la Mvumoni Mfikiwa katika wilaya ya Chake-Chake kujipanga upya ili kuhakikisha soko hilo linafanya kazi kama walivyo omba kujengewa.
Alisema endapo kamati hiyo itashindwa kujipanga upya na soko hilo kufanya kazi kama lilivyo kusudiwa baada mwezi moja baadhi ya vifaa viliomo kama vile mafriza ya kuhifhadhia samaki ndani ya soko hilo atavikabidhi kwa vikundi vilivyomo ndani ya Shehia nyengine iliwaweze kuvifanyia kazi ambavyo wao wana vihitaji.
Hayo aliyasema huko Mvumoni Mfikiwa wakati alipokuwa akizungumza na kamati ya soko hilo kufuatia kushindwa kufanya kazi kwa soko hilo ambalo ujenzi wake uligharimu zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka msada wa MACEMP.
“Jamani mimi na kushangaeni watu wana lilia soko kwa maendeleo yao, kila mmoja anajua soko ni usitawi, soko ni biashara soko ni uchumi ni maendeleo nyinyi mnaliacha hivi hivi tu”, alisema waziri huyo.
Alisema kama wananchi wa Mvumoni wange jipanga na kujaza bidhaa zinazo patikana kijijini na hata za kutafuta kutoka maeneo ya mbali ingetoa nafasi kwa soko hilo kuwa kituo cha bidhaa ambacho kingetumiwa hasa na wasafiri wanao tumia uwanja wa ndege wa Karume kwa kuchukua zawadi za Pemba sokoni hapo.
Waziri huyo alisema wananchi wa Mvumoni waliomba wenyewe kujengewa soko hilo hivyo hawana sababu ya kutolitumia kama walivyo omba.
Mapemba Mkuu wa wilaya Chake-Chake, Mwanajuma Majidi Abdalla alisema kuwa kutofanya kazi kwa soko la kunatokana na kamati ya soko hilo kutokuwa makini kwani alikwisha waita mara kadha kuzungumza nao lakini hadi sasa wameshindwa kubadilika na kuliwacha bila kulitumia.
Alishauri kuondolewa kwa kamati iliyopo na kuwekwa kwa kamati nyengine ili lengo la kufanya kazi kwa soko hilo iweze kupatikana kama ilivyo kusudiwa.
Kwa upande wao baadhi ya wanakamati hao walimuomba waziri kuachiwa kuendelea ilikufanya mabadiliko yatakayo saidia kuboresha nakuweza kufanya kazi kwa soko hilo. Hata hivyo moja kati ya vijana walio kuwepo kwenye mkutano huo alidai kuwa hakuna kamati inayo endesha soko hilo na kwamba mara baada ya kumaliza kazi ya ujenzi kwa kamati kilicho endelea ni wazee kuhodhi soko ambalo lipo yao.
No comments:
Post a Comment