Habari za Punde

HAKUNA SABABU WAWEKEZAJI MAKINI KUKATALIWA- BALOZI SEIF

Na Abdulla Ali, OMPR

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameeleza kufurahishwa kwake na  nia ya wawekezaji wa Kampuni ya mawasiliano ya habari ya STS SMART TECH  Solution ya Uingereza ya kutaka kuwekeza Zanzibar.


Balozi Seif aliyaeleza hayo alipozungumza na Uongozi wa kampuni hiyo ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Hussein Abdulkader, ulipofika ofisini kwake Vuga kusalimiana naye.

Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikitafuta wawekezaji kutoka kila pembe ya dunia kuwekeza, haoni sababu ya wawekezaji makini kukataliwa iwapo watafuata taratibu zilizowekwa.

Kwa hivyo aliwataka wawekezaji hao kufuata taratibu hizo kwa kupitia mamlaka ya uwekezaji (ZIPA) kwa lengo la kupata maelekezo ya kisheria ya uwekezaji na kuahidi kuwa Serikali iko pamoja nao.

Kwa upande wake kiongozi wa ujumbe huo alisema Kampuni yao ikipata ridhaa ya kuwekeza inakusudia kuweka mitambo ya kisasa ya Internet yenye spidi kubwa itayoweza kutumika nchi nzima kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Aidha alisema matumizi ya mtandao wao huo utasaidia sana kuimarisha mawasiliano katika Taasisi za Serikali na watu binafsi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.