RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa serikali iliyopo madarakani chini ya uongozi wake itahakikisha inayaangalia maslahi ya wafanyakazi hatua kwa hatua kwa mujibu hali ya kiuchumi itakavyoruhusu.
Dk. Shein ambaye pia, ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliyasema hayo leo huko Mkokotoni katika ukumbi wa Chuo Cha Amali wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini A.
Katika maelezo yake hayo Dk. Shein alisema kuwa serikali yake itachukua hatua hiyo ya kuangalia maslahi ya wafanyakazi kwa kutambua mchango wao mkubwa katika ujenzi wa taifa hili.
Aidha, Dk. Shein aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo ambao ni viongozi wa CCM Wilaya ya Kaskazini A kuwa katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba ameweza kujionea namna ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo.
Alisema kuwa suala zima la ajira litapewa kipaumbele na kueleza kuwa juhudi zitachukulwia katika kuhakikisha suala la ajira kwa vijana linapewa kipaumbele.
Aidha, Dk. Shein alieleza mafanikio yaliopatikaka katika sekta ya elimu ambapo alieleza kuwa tayari hatua kubwa zimefikiwa katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa skuli mpya za kisasa za Sekondari Unguja na Pemba.
Alieleza kuwa katika suala la elimu ujenzi wa skuli hizo katika hiyo pia unakwenda vizuri sambamba na uimarishaji wa sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kupanua huduma za akina mama na watoto, huduma za meno na huduma nyenginezo.
Aliwapongeza viongozi wote wa Mkoa pamoja na Wilaya ya Kaskazini Unguja na kueleza lengo la serikali la kuipandisha daraja hospitali ya Kivuge na kusisitiza kuwa katika kipindi kifupi kijacho hudma za afya zitabadilika kwa kasi.
Alisisitiza haja ya kupiga vita suala la ubakaji na kurejea kauli yake aliyoitoa wakati wa ziara yake katika Mkoa huo ya kufanya utafiti kutokana na kadhia hiyo ambapo watoto wadogo wamekuwa wakifanyiwa uharibifu mkubwa kwa lengo la kutafuta mtaalamu wa Sosolojia.
Alieleza kuwa kutokana na tabia hiyo Chama Cha Mapinduzi na Serikali inayoiongoza hakifurahishwi na kusisitiza haja ya kupigwa vita kwa kiasi kikubwa tatizo hilo, na viongozi wanapaswa kulisimamia vyema.
Alisisitiza suala zima la mazingira, na kuwataka viongozi kusimamia mazingira kwani kuna hatari kubwa iwapo mazingira yataharibiwa ambapo tayari baadhi ya sehemu Unguja na Pemba zimeshaanza kuathirika na hali hiyo kutokana na hali nzima ya tabia nchi.
Alileza kuwa ziara yake ya Mikoa mitano ya Unguja na Pemba ilikuwa na mafanikio makubwa katika muelekeo mzima wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusema kuwa mambo mazuri yameanza ikiwa ni pamoja na kutekelezwa kwa kasi nIlani hiyo.
Akieleza juu ya ali ya maisha Dk. Shein alisema kuwa tatizo hilo ni la dunia nzima hali ambayo inatokana na mfumko wa bei za vyakula duniani ambako wazalishaji wengi wa vyakula wamepandisha bei za bidhaa hizo kutokana na mabadiliko ya uchumi.
Juu ya suala hilo Dk. Shein alisema kuwa serikali haikukaa kimya na inafanya kazi na jitihada zimo mbioni kufanywa ikiwa ni pamoja na kuimarisha seka ya kilimo hasa kilomo cha mpunga wa umwagkiaji maji.
Aidha, alisema kuwa serikali imeamua kwa makusudi katika kipindi kifupi kijamcho kulima hekta 6000, ambapo juhudi zitachukuliwa katika kuhakikisha huduma za maji, elimu, matrekta, mbegu, dawa na pembejeo.
Alieleza kuwa yale yote aliyoyaahidi yatatekelezwa hatua kwa hatua na kusisitiza kuwa Dira ya 2020 madhumnuni yake hasa ni kuwatoa wananchi wa Zanzibar katika umasikini wa kipato na kuwa na uwezo wa kipato na tija.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza haja ya viongozi kuwa na ari ya kujitolea katika kuimarisha miradi ya maendeleo na huduma za maendeleo.
No comments:
Post a Comment