6/recent/ticker-posts

Rais Dk Hussein Mwinyi mgeni rasmi Ufunguzi wa Uwanja wa Gombani



 Wilaya ya ChakeChake Pemba 13.01.2026.


Ujenzi na Ukarabati wa Viwanja mbalimbali vya Michezo ni miongoni mwa juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika  kuimarisha Michezo Nchini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Uwanja wa Gombani baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa sambamba na fainali ya NMB Mapinduzi Cup 2026.

Dkt. Mwinyi ameuhakikishia Umma kuwa, Serikali itaendelea kujenga na kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Michezo katika Wilaya na Mikoa ili kuibuwa Vipaji ambavyo vitaiwakilisha Nchi kitaifa na kimataifa.

Aidha ameipongeza Wizara ya Habari, Sanàa, Utamaduni na Michezo kwa kufanya kazi nzuri ya kusimamia Ujenzi wa Viwanja vya Michezo na kufikia malengo yaliokusudiwa na Serikali.

Nae Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma amesema miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ni kuhakikisha inaimarisha viwanja vya michezo Nchini.

Fainali za NMB Mapinduzi Cup, imefanyika katika Kiwanja cha Gombani Chakechake Pemba ambapo kwa mwaka 2026 Timu ya Yanga imetwaa Kombe hilo baada ya kuichapa Azam Fc kwa Mikwaju ya Penalti 5 kwa 4.

Mshindi wa Kwanza katika Kombe hilo, amekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo Kitita cha Sh. milioni 150 na Mshindi wa pili Sh. Milioni 10.

Imetolewa na Kitengo cha Habari,

WHSUM.

Post a Comment

0 Comments