6/recent/ticker-posts

Serikali kuunda timu ya wataalamu kutatua suala la ajira


 Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe. Shaaban Ali Othman, amezungumza na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali za SMZ ili kujadili fursa na mikakati ya upatikanaji wa Ajira kwa Vijana huko katika Ukumbi wa BLM Maisara Wilaya ya Mjini

Wilaya ya Mjini.                  14.01.2026.

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe. Shaaban Ali Othman amewataka Makatibu wakuu wa Wizara za Serikali ya SMZ, kushirikiana ili kutafuta suluhu ya changamoto ya Ajira kwa Vijana.

Akizungumzaa katika kikao cha kujadili fursa na mikakati ya upatikanaji wa Ajira kwa Vijana huko Maisara Wilaya ya Mjini amesema mashirikiano hayo yatasaidia Serikali kuwawezesha Vijana katika Soko la Ajira.

Amesema Wizara, imeunda Timu ya Wataalamu wa kuandaa mpango mikakati, utakaoweza kuleta majibu kuhusu suala la Ajira.

Hivyo amesema mashirikiano yao, yatapelekea kufikia Azma ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuwakomboa Vijana Kiuchumi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Salama Mbarouk Khatib ameahidi kushirikiana na Taasisi za Serikali na binafsi, zinazotoa Ajira ili Vijana Wazalendo waweze kufaidika na fursa mbalimbali zikizopo.

Nao Baadhi ya Viongozi hao, wameahidi kushirikiana na Serikali katika kuongeza idadi ya Vijana watakaoweza kushiriki katika Soko la Ajira Nchini.

Imetolewa na Kitengo cha Habari,

WVAU.

Post a Comment

0 Comments