Habari za Punde

AJALI YA MELI LATEST UPDATE

Mpaka tunawarushia taarifa hizi ni kwamba leo zimeweza kupatikana maiti nyengine 5 na hivyo kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 197. Hakuna aliyepatikana akiwa hai.

Pia kuna maiti nyengine 28 zimezikwa leo na Serikali maeneo maalum ya Kama na hivyo kutimiza watu 45 ambao tayari wameshazikwa na Serikali.

Idara ya Maafa imetoa taarifa rasmi kwamba maiti yeyote itakayopatikana kuanzia sasa itashughulikiwa na Serikali na hivyo itazikwa na kushughulikiwa na Serikali moja kwa moja.

Pia wananchi wote ambao wana wasiwasi na hatima za jamaa, ndugu zao ambao bado hawajapatikana au kuonekana wametakiwa kwenda Idara ya Maafa kuorodhesha majina ya jamaa zao kwa ufuatiliaji wa karibu zaidi.

Kesho jioni baada ya Sala ya Alasiri kutakuwa na dua maalum itakayosomwa kuwaombea wafiwa pamoja na waathirika wote kwa ujumla katika viwanja vya Maisara

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.