Habari za Punde

BALOZI SEIF ALIPOSHUHUDIA MANDALIZI YA KUPOKEA MAITI, MAJERUHI


NI WATU WALIOJAZANA KUANZIA UWANJA WA MAISARA HADI HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA WAKISUBIRI KUWATAMBUA MAITI ZAO KARIBU MATAYARISHO YOTE YANAYO STAIKI KUFANYIWA MAITI YAMEKAMILIKA KINACHOSUBIRIWA NI UPOKEAJI WA MAITI, TAYARI WATU WASIOPUNGUA 300 WAMEOKOLEWA WAKIWA WAZIMA WENGI WAO NI WATOTO NA KINAMAMA
BALOZI SEIF ALI IDDI AKITOA MAELEKEZO JUU YA UTARATIWA WA KUFUATWA KWA WATU WATAKAOKUJA KUANGALIA MAITI ZAO NDANI YA HEMA, HADI MUDA HUU TAYARI MAITI MBILI ZIMESHA HIFADHIWA NDANI YA HEMA ILO TAYARI KWA KUTAMBULIWA KATIKA MAANDALIZI HAYO IDARA YA MAAFA WAKISHIRIKIANA NA OFISI YA MUFTI WA ZANZIBAR WATAZIHUDUMIA MAITI ZOTE KWA KUZIKOSHA,KUZIFIKA SANDA NA KUZIKA

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE, BALOZI SEI ALI IDDI AKIONGOZWA NA NAIBU KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEKHE KHAMIS HAJI KHAMIS WAKITOKA NDANI YA HEMA MAALUM LILILOJENGWA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA KWA AJILI YA KUPOKELEA MAITI ZA AJARI YA MV.SPICE ISLANDERS ILIOKUWA IKITOKEA UNGUJA KWENDA PEMBA USIKU WA JANA.#

PICHA NA OFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.