Habari za Punde

KISOMO KUWAOMBEA NA KUSAIDIA KUCHANGIA WAATHIRIKA AJALI YA MV SPICE KILICHO SOMWA NA JUMUIYA YA KIISLAMU TAMCO - MAREKANI




Vitabu vya hitma vilivyo tumika  kwenye kisomo cha kuwaombeakuwapa pole wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali ya meli ya Mv Spice iliotakea Tanzania Zanzibar siku ya Ijumaa kumakia jumamosi ya September 10/2011


Waumini wa Kiislamu wakisali sala ya kuwaombea wale wote waliofariki katika ajali ya Mv Spice iliotokea Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja



Mh Abass Misana, picha ya wa kwanza (Kulia) pamoja na Ofisa wa Ubalozi hapa Washington DC Mh Suleiman Saleh wakiwa katia kisomo kilichosomwa leo Jumapili Sep18,2011 katika ukumbi wa New Hampshire Avenue, Silver Spring,MD Nchini Marekani.



Baadhi ya Watanzania waliohudhuria katika dua pamoja kuchangia kukusanya fedha ilikuweza kuzisaidia familia zilizopoteza ndugu pia kusaidia shughuli zote za mazishi kwa wale waliofariki





Kina dada mbali mbali waliohudhuria katika dua hiyo pampja na Harambee ya kuchangia walioathirika kwenye ajali ya meli ya Mv Spice iliotakea Tanzania Zanzibar siku ya Ijumaa kuamkia jumamosi ya September 10/2011


Kiwango cha fedha kilichopatikana katika shughuli hiyo ni Us Dollars 4000/- kutokana na mauzo na baadhi ya vitu tofauti vilivyoletwa na Watanzania kwa ajili ya kuchangia fedha ilikuweza kuzisaidia familia zilizopoteza ndugu pia kusaidia shughuli zote za mazishi kwa wale waliofariki. Picha zotekwa hisani ya  www.swahilivilla.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.