JUMLA ya shilingi 145,045,890 zimetolewa Walimu wa serikali kwa ajili ya kuchangia sherehe na Matamasha ya Elimu yanayofanyika kila mwaka.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Hamad aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Mahmoud Muhammed Mussa alietaka kujua namna ya michango hiyo inavyotumika kwa kuwapo taarifa za matumizi mabaya ya fedha hizo huku kukiwa na utaratibu wa kuwakata walimu fedha hizo bila ya ridhaa yao.
Akijibu suala hilo Naibu huyo alisema kiasi hicho cha fedha kilikusanywa katika kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010 ikiwa ni michango inayotolewa kwa njia ya hiyari na serikali imekuwa na utaratibu wa kuzifanyia ukaguzi kwa kutumia wakaguzi wa ndani na nje wa mahesabu ya serikali.
Alisema fedha hizo zimekuwa zikikatwa kutoka kwa walimu pale wanapoombwa kufanya hivyo, wakiwa pamoja na michangi ya wananchi ambao hujitolea kuchangia.
Hata hivyo Naibu huyo alisema Wizara hiyo haina taarifa ya kuwepo kwa mikato iliyofanywa kwa kutoa asilimia mbili ya mishahara yao kwa baadhi ya walimu wa Micheweni na Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba ambapo walikatwa shilingi 500.
Alisema anachofahamu ni kuwepo kwa michango iliyotolewa na Walimu wa Wilaya ya Kusini Unguja kwan ajili ya ujenzi wa Afisi ya Elimu ya Wilaya hiyo ambapo michango hiyo ilitolewa kwa ridhaa yao biloa ya kuishirikisha Wizara.
Naibu huyo pia alikataa kama maafisa waandamizi wa Wizara hiyo ambao hutumia fedha hizo bila ya kufuata taratibu za kanuni za matumizi ya fedha.
Hata hivyo Naibu huyo alikubali kuona fedha hizo hivi sasa ziwe zinaingizwa katika bajeti ya Wizara hiyo ili kuweza kuweka uwazi wa matumizi ya fedha hizo.
Mtu mzima haitwi muong...lkn uuh! hivi kuna mwlimu anaekubali kukatwa mshahara ili kuchangia tamasha? ..labda siku hizi!
ReplyDelete