Habari za Punde

KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR ILIVYOKUTANA

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,pia Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amaani Abeid Karume,akiendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Zanzibar,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk Ali Mohamed Shein,
Baadhi ya wajumbe wa CCM wa Kikao cha kamati maalum ya Halamashauri kuu ya CCM Zanzibar, wakisikiliza mada zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi kuu ya Chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar
Baadhi ya wajumbe wa CCM wa Kikao cha kamati maalum ya Halamashauri kuu ya CCM Zanzibar, wakisikiliza mada zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi kuu ya Chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,katika viwanja vya Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipohudhuria kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM jana.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,pia Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amaani Abeid Karume, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yussuf Mohamed ,alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui kuendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo jana.
Rais Mstaafu wa Tanzania,pia Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mzee Ali Hassan Mwinyi, akisalimiana na viongozi wa CCM Ofisi ya chama hicho Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo jana kilifanyika kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi,aliposalimiana na Viongozi wa CCM Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, alipohudhuria kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri kuu ya chama hicho,kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Ofisi hiyo Mjini Zanzibar

Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.