Habari za Punde

MAHAFALI YA SABA YA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA)

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo hicho hawapo pichani kabla ya kuwatunuku shahada zao katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Profesa Idrisa Rai akitoa muhtasari wa Chuo cha Suza katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume ambae alitunukiwa shahada ya uzamivu akizungumza katika Mahafali ya Saba leo.
Wakuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Dk Shein (kulia) Profesa Idrisa Rai (katikati) na Ismail Kanduru (kushoto)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimtunuku shahada ya uzamivu ya heshima ya chuo kikuu cha Taifa SUZA Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume,wakati wa sherehe za mahafali ya 7 ya chuo hicho katika viwanja vya Mnazi mmoja Mjini Unguja.



Mkuu wa Chuo cha Suza DK Shein akimkabidhi zawadi Said Salim Bakhresa kwa mchango wake mkubwa kukisaidia Chuo hicho katika mahafali ya sabayaliyofanyika leo








Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA wakisubiri kutunukiwa Shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
Viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais, Raisi Mstaafu, Mawaziri pamoja na Manaibu na Makatibu walikuwepo katika mahafali ya Saba a Chuo kikuu cha Suza

1 comment:

  1. Ahsante kwa picha ndio maana ninapokua mbali na nyumbani nakuchagua mapara kwa habari za nyumbani. Ahsante pia kwa kazi nzito unayotufanyia

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.