Habari za Punde

WAKULIMA WA KARAFUU WAKUSANYA 42.859/- BILIONI KWA MIEZI SITA

Na Hafsa Golo

SHIRIKA la Biashara la Taifa ZSTC limetumia shilingi bilioni 42.859 kununua zaidi ya tani 2800 za karafuu kutokla kwa wakulima mbali mbali Unguja na Pemba Julai 5 mwaka huu.

kutoka kwa wakulima zikigharimu jumla ya shiling 42.859 bilion tokea msimu wa zao la karafuu kuanza julai 5,2011.

Meneja Mkuu wa shirika hilo, Suleiman Juma Jongo alitoa takwimu hizo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Maisara, mwishoni mwa wiki. Alisema kati ya karafuu hizo, shirika lake limesafirisha nje ya nchi kwa kuuza tani 1800 za zao hilo.


Alisema karafuu hizo zimeuzwa katika nchi mbali mbali ikiwemo Indonesia, India ,singapure na Dubai Hata hivyo, alisema anaanini shirika la Biashara la Taifa litaendelea kununu karafuu hadi msimu wa vuli utakapomalizika kwa vile karafuu nyingi bado ziko mikarafuuni hazijachumwa.

Meneja huyo aliwataka wananchi waendelee kuuza karafuu zao ZSTC ili serikali iweze kuinua uchumi wake na kuiwezesha kumudu gharama za uendeshaji na kutoa huduma mbali mbali kwa wananchi kupitia fedha zitokanazo na biashara hiyo.

Huduma hizo ni pamoja na kugharamia afya, elimu pamoja na kukuza biashara nchini.

Hata hivyo, alisema suala la magendo ya karafuu, serikali imejitahidi kupiga vita biashara hiyo kwa kuunda kikundi kazi kushughulikia zao la karafuu na wananchi wenyewe wameitikia wito na kujenga uzalendo kwa kuziuza kupitia shirika hilo.


Pamoja na hayo alisema Unguja zao la karafuu limeanza kununuliwa kwa kasi hivi sasa na kufikia tani 179 ambazo zimegharimu bilioni 2.6 hata hivyo alifahamisha kuwa msimu wa zao la karafuu Unguja hushamiri wakati wa wavuli.

Aidha, Jongo alisema ni upuuzi mtupu madai kwamba Shirika lmekuwa likinunua karafuu kutoka kwa wananchi kwa njia za mkopo na wala halina dhamira hiyo.


''Utaratibu uliopo hakopwi mtu, hili ni suala la uzushi wanasema tu hakuna ukweli wowote,'' alifafanua Jongo.

Meneja Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa zao hilo kuanikwa kwa kutumia majamvi na kuzisafisha na kuhakikisha zinakauka kabla ya kupeleka vituo vya mauzo ili kuepuka kufanya kazi hiyo mara mbili kwenye vituo vya ununuzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.