Na Ali Bakari
TIMU ya Mafunzo, jana imemaliza mechi za kundi B za mashindano ya Kombe la Mapinduzi, kufuatia ushindi wa bao 1-0 mbele ya wanyonge Kikwajuni.
Bao la Mafunzo lilipatikana katika dakika ya 59, likifungwa na Sadik Habib baada ya wachezaji wa timu hiyo kugongeana vyema mpira. Mjini, Kaskazini A zashinda
Kwa ushindi huo, Mafunzo imetinga hatua ya nusu fainali, na ilitarajia kujua imershika nafsi ya ngapi bada ya mchezo mwengine wa kundi hilo kati ya Yanga na Azam FC, uliotarajiwa kuchezwa jana usiku.
NAYE HADIA KHAMIS, anaripoti kuwa, katika michuano kama hiyo ngazi ya Central kwa kombaini za wilaya, ‘Abed Amani Karume Cup’, Kaskazini B ilishindwa kuutumia vyema uwanja wake na kufungwa 2-0 na Wilaya ya Mjini katika uwanja wa Mahonda.
Na katika uwanja wa Mkwajuni, timu ya Wilaya ya Kaskazini A, ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wilaya ya Kati.
No comments:
Post a Comment