6/recent/ticker-posts

Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya BLW yakagua vivutio vya utalii



Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo imesisitiza haja ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kuendelea kuviimarisha Vivutio vya Utalii ili vizidi kuwavutia wageni wa ndani na nje ya Zanzibar.
Hayo yameelezwa na Wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Fatma Ramadhan Mohamed baada ya kupokea taarifa ya Kamisheni ya Utalii na kufanya ziara fupi ya kutembelea Vivutio mbali mbali vya Utalii vilivyopo Nchini.
Aidha ziara hiyo iliongozwa na Wenyeji akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dkt Aboud Suleiman Jumbe na Wakurugenzi kutoka Taasisi mbali mbali za Wizara ikiwemo Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Zanzibar na Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe.


 

Post a Comment

0 Comments