6/recent/ticker-posts

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akutana na Ujumbe kutoka Kampuni ya Condor ya Brazil


 

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma amekutana na Ujumbe kutoka Kampuni ya Condor ya Brazil wakati walipofika Ofisini kwake Migombani Wilaya ya Mjini.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma, leo ameeleza kuridhishwa na ujio wa Kampuni ya Condor kutoka Nchini Brazil.

Akizungumza na Viongozi wa Kampuni hiyo waliofika Ofisini kwake kujitambulisha amesema Kampuni hiyo, inajishughulisha na Uuuzaji wa Vifaa vya Ulinzi katika sekta mbalimbali ikiwemo Michezo.

Amesema Kampuni hiyo, imeonyesha nia ya kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Michezo katika kupeleka mbele Maendeleo ya Ulinzi na Usalama hususan kwenye Michezo.

Aidha amesema, Kampuni hiyo imeuza vifaa katika Nchi 48 Duniani ikiwemo, Algeria na Morocco.

Kwa upande wa Viongozi wa Ujumbe huo, wamempongeza Dkt. Riziki kwa mapokezi mazuri alioyaonyesha na kuahidi kushirikiana kwa maslahi ya pande zote mbili (Serikali na Kampuni).

Hata hivyo wamesema lengo kuu la Taasisi yao ni kuuza vifaa hivyo ili kulinda maisha ya Wanadamu.

Hata hivyo wamesema, pia wanatoa mafunzo ya ulinzi na Usalama ambapo walishawahi kutoa kwa Watendaji wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar.

Miongoni mwa Viongozi wa Taasisi hiyo waliohudhuria ni pamoja na Mwakilishi wa Ubalozi wa Brazil nchini Tanzania Luciana Teixeira, Mtendaji wa Masoko ya kimataifa Kareem Seklawi na Meneja Masoko ya kimataifa Renan Annize. 

Imetolewa na Kitengo cha Habari,

WHSUM.

Post a Comment

0 Comments