Habari za Punde

Wanawake Washauriwa Kusaidiana Kimaendeleo


Na Fatma Omar, WKUU

KATIBU Mkuu wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Asha Ali Abdalla amewataka wanawake kusaidiana na kujishughulisha katika harakati za kiuchumi zitakazowaletea maendeleo.

Katibu huyo alieleza hayo wakati akimkabidhi fedha aliekuwa mshindi wa pili wa Tanzania katika shindano la mama shujaa wa chakula Mwandiwe Makame Kali.


Fedha alikabidhiwa ikiwa ni ahadi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwenye maadhimisho ya wiki ya uwezeshaji, huko katika ofisi Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.

Alisema lengo la fedha hizo ni kuongeza nguvu na juhudi katika kazi za maendeleo pamoja na kusaidia kujiendeleza zaidi na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Katibu huyo alifahamisha kuwa mafanikio hayo yawe chachu ya kuweza kuleta maendeleo kwa wanawake wengine, pamoja na kuwa balozi wa kuwahamasisha waweze kushiriki katika mashindano mbalimbali ndani nje ya nchi.

Kwa upande wake Mwandiwe alisema fedha alizopewa atatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na pia kuwahamasisha wanawake katika washiriki shindano la mama shujaa la Tanzania.

Aidha alisema ameweza kutokea mshindi pili kutokakana na juhudi alizokuwa akizifanya huku akiwa amejikimu chakula cha nusu mwaka ambapo anatarajia apambane zaidi aweze kujikimu aweze cha mwaka
mzima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.