Habari za Punde

Bwejuu Bingwa Kombe la Ushirikiano

Na Haroub Hussein

TIMU ya soka ya Bwejuu, imeibuka bingwa wa Kombe la Ushirikiano kwa changamoto ya mikwaju ya penelti 4-1 dhidi ya majirani zao Michamvi, katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kiganya Bwejuu.

Hatua ya kupigiana penelti ilikuja baada ya wanaume hao kuzitafuna dakika 90 za mchezo wakiwa sare ya 2-2.

Michamvi ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuzifumania nyavu za majirani zao katika dakika ya 28, kwa bao lililofungwa na Khalid Kheir, kabla Bwejuu kuchachamaa na kusawazisha mnamo dakika ya 40 kupitia kwa
mchezaji Khamis Haji.


Salum Machano wa Michamvi alifanikiwa kupachika bao la pili katika dakika ya 46, huku Mohammed Abdallah akiifariji Bwejuu kwa bao la pili kwenye dakika ya 54.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa pambano hilo, mgeni rasmi Mkurugenzi wa Hoteli za Breeze Beach Club na Baraza Spa Hassan Gharib, aliwataka wanakijiji hao kudumisha umoja na mshikamano ikiwa ni njia
ya kuwawezesha wawekezaji kuweza kufanya biashara zao kwa hali ya utulivu.

Gharib alisema wawekezaji wako tayari kusaidia miradi mbalimbali katika vijiji wanavyofanyia kazi, kwa lengo la kuwainua kimaisha wanavijiji ili nao waweze kuilinda na kushirikiana.

Kwa kutwaa ubingwa, timu ya Bwejuu ilikabidhiwa kitita cha shilingi lake nane na kikombe, huku Michamvi iliondoka na shilingi laki nne kwa kushika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.