Habari za Punde

Manchester yakunjua mbawa

LONDON, Uingereza

USHINDI wa magoli 2-0 dhidi ya QPR ambao Manchester United iliupata jana katika pambano la ligi kuu ya England, uliiwezesha kuendelea kutanua kileleni mwa msimamo kwa tafauti ya pointi nane dhidi ya wapinzani wao wa karibu Manchester City.

Hata hivyo, City iliyotarajiwa kuivaa Arsenal baadae jioni ya jana, ilikuwa na uwezo wa angalau kupunguza pengo kama ingeweza kuishinda Gunners au kuambulia sare.


Pamoja na kutawala mchezo huo, United pia ilinufaika sana na makosa makubwa yaliyofanywa na muamuzi wa pambano hilo Lee Mason.

Ilionekana wazi kuwa kulikuwa na mgongano mdogo kati ya wachezaji hao, lakini Mason aliashiria kupigwa penelti bila kwanza kumuuliza msaidizi wake huku akimuamuru Derry kutoka nje kwa kumzuia Young asifunge bao.

Mshambuliaji wa United Ashley Young, alionekana wazi kuwa ameotea wakati alipogongana na kiungo Shaun Derry wa QPR katika dakika ya 14, na hivyo muamuzi huyo kuizawadia United mkwaju wa penelti uliopigwa na Wayne Rooney kuiandikia timu yake bao la kwanza.

Baadae mnamo dakika ya 68, jitihada za Scholes zilimuwezesha kupachika bao la pili na kuwawezesha wekundu hao kujipatia ushindi wa nane mfululizo kwa mara ya kwanza tangu ligi ya mwaka 2009.

Hata hivyo, United haiku katika hatari kubwa mbele ya wachezaji kumi wa QPR baada ya Derry kutolewa nje, ambapo Scholes aliweza kutumia nafasi hiyo kuachia shuti la nguvu kutoka umbali wa yadi 25 lililomuacha mlinda mlango Kenny akiruka bila mafanikio dakika 22 kabla mchezo kumalizika.

Kwa matokeo hayo, kikosi hicho cha Mark Hughes kinabaki katika nafasi ya nne kutoka mkiani mbele ya Wigan na Blackburn Rovers kwa tafauti ya mabao huku timu zote hizo zikikabiliwa na hatari ya kushuka daraja.

Watoto hao wa Malkia wamemudu kuambulia pointi mbili tu katika mechi tisa za mwisho walizocheza ugenini katika ligi hiyo tangu waliopoifunga Stoke City mabao 3-2 mwezi Novemba. (Eurosport).

2 comments:

  1. Manchester United imecheza leo tarehe 8/4/2012 na sio jana.Na mpaka na comment hii report bado ni tarehe 8/4/2012.

    ReplyDelete
  2. Wacha ikunjue! na sisi'The gunners' tumezidi kuwasafishia njia kwa kuwapiga City 1-0!..huku Yaya toure, knee injury na Balloteli red card!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.