Joseph Ngilisho, ARUSHA
NABII Benjamin Asaf ameanguka hafla kanisani wakati akioendesha sala ya kuwaombea laana waandishi wa habari na waumini wa kanisa lake.
Nabii huyo wa kanisa la huduma ya mti wa uzima madhehebu ya
Ebenezer Gospel Church lilioko Mererani, alikuwaa akiendesha sala ya kuwaombe
waumini wake waliotoa habari kwa waandishi juu ya kadhia ya kuwanyanyasa na
kupiga teke sadaka akidai kidogo.
Aidha sala hiyo pia ililenga kuwaombea laana waandishi wa
habari waliojitia kimbelembele cha kuandika habari hizo, ambapo kabla ya
kumaliza sala hiyo alidondoka chini.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa sharti la kutotajwa
majina yao, waumini hao walisema kuwa mchungaji huyo alianguka ghafla kwenye
madhabahu ya kanisa hilo.
Walisema wakatia kiingia kanisani alikuwa akisema leo kazi
ni moja tu ya kuendesha maombi ya kuwalaani waandishi wa habari wote walioandika
habari zake.
“Wakati akiendelea kuomba huku akiwa ameshikilia bibilia
ghafla alianguka chini na kupoteza fahamu kwa muda na baadae waumini hao
walimpepea ambapo aliinuka ila hakuendelea tena na maombi”,alisema mmoja wa
waumini aliyekuwepo kanisani hapo.
Waumini hao walisema inawezekana laana aliyokusudia iwafike
waandishi wa habari na baadhi ya waumini waliovujisha siri za kanisa hilo juu
ya kadhia ya kuvunja madhabahu na kupiga teke kikapu cha sadaka, imemrejea
mwenyewe.
Waumini hao walisema mhubiri huyo anayejiita nabii, amewatendea
kosa kubwa kupiga teke sadaka zao walizozitoa kwa ajili ya Mungu na kuvunja
madhabahu yao.
Aidha walisema nabii huyo aliwatolea maneno ya ujeuri baada
ya kuvunja madhabahu kwa kuwataka mabaki wakapikie makande na kueleza kuwa
sakada wanazotoa kidogo ndio maana mchungaji wao Joshua Baraka hanenepi.
Wamesema katika ibada iliyofanyika wiki iliyopita kwenye
dhehebu lao Nabii huyo aliwaita waumini hao wadudu, kunguni na mende na kuwauliza kuwa kwanini walipeleka
jambo hilo kwenye vyombo vya habari.
Mmoja kati ya waumini hao ambaye alikuwa na mtoto mdogo
wakati tukio hilo linafanyika alisema alisikia uchungu kuona sadaka aliyoitoa
kwa ajili ya Mungu kwanini ipigwa teke.
Alisema wakati Nabii huyo akipiga teke kapu la sadaka, noti
ya shilingi 1000 ilimrukia mguuni mwake ndipo alipoamua kuichukua na kuiweka
kwenye pochi na kuamua kuhama kanisa hilo na hadi hivi sasa amehamia kanisa la
huduma ya Haradali.
Hata hivyo, waumini hao wameshangazwa na kitendo cha wao
kusimangwa na na mtu huyo anayejiita nabii na kudai kuwa wao wamenenepeana huku
mchungaji wao Baraka Joshua akiwa amekonda.
Walisema uongozi wao unatakiwa kugeuka kwani kitendo hicho
cha kupiga teke sadaka na kuvunja madhabahu kinafanana na waamini wa kule Mbeya
ambao hivi karibuni nao walivunja madhabau yao wakitafuta madini
yaliyohifadhiwa na wamisionari.
No comments:
Post a Comment