Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa
madrasat Nurullah Kitope Zanzibar,iliyopo Wilaya ya Kaskazini B
Unguja,Mkoa wa Kaskazini,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi,jengo
hilo limejengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi,
chini usimamizi wa mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza
.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akifuatana Makamo wa Pili wa Rais
wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali
Iddi,pamoja na viongozi wengine alipowasili katika Jengo la Madrasat
Nurullah Kitope,kwa ajili ya kulifungua rasmi,lililojengwa kwa
ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. [Picha na
Ramadhan Othman Ikulu.]
Baadhi ya wanafunzi wa Kiume wa Madrasat Nurullah ya Kitope
wakiwa mbele ya uwanja wa jengo la Madrasa yao baada ya kufunguliwa
rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj
Dk.Ali Mohamed Shein,jana .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wa pili kushoto) akipokea risala ya
wananchi na wanamadrasat Nurullah ya Kitope Wilaya ya Kaskazini B
Unguja,kutoka kwa Mwalimu Juma Mohamed,baada ya kuifungua Madrasa hiyo
jana,iliyojengwa na Abdalla Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi
wa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. [Picha na Ramadhan
Othman Ikulu.]
No comments:
Post a Comment