Habari za Punde

Wawili Waenda Iran Kushindana Kuhifadhi Qur'aan


Na Fatuma Kitima, DAR ES SALAAM
WATANZANIA wawili wanatarajia kushriki mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Quran yanayotarajia kufanyika Jamhuri ya Kiislam ya Iran.

Washiriki hao watakaoipeperusha bendera ya taifa nchini Irani ni pamoja na Said Said kutoka Tanzania bara aliyehifadhi juzuu 30 na Omar Abdallah Salim ambaye naye amehifadhi juzuu 30.

Mashindano yanayofanyika kila mwaka nchini humo huandaliwa kituo cha utamaduni cha Jamuhuri ya Iran, ambapo kwa mwaka huu vijana hao wawili ndiyo wanayoiwakilisha nchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu wa Mkoa huo Alhad Mussa Salum wakati wa hafla ya kuwaaga vijana hao watakaoshiriki mashindano hayo ambayo yatachukua muda wa wiki moja.


Alisema vijana hao walipatikana katika mchujo ulioshirikisha mikoa yote nchini kuanzia ngazi ya wilaya.

Sheikh Salum alisema lengo la mashindano hayo ni kuwalea katika maadili mema yanayopendeza mbele ya Mwenyezi mungu pia katika jamii inayowazunguka.

"Mchujo ulianza katika wilaya, mikoa hivyo tulipata wawakilishi sita toka kila kanda, baada ya mchujo huo tulipata wawakilishi hawa watakoenda kuiwakilisha kwenye mashindano hayo ya kimataifa,"alisema Sheik Salum.

Aliwataka vijana wengine waongeze juhudi katika kuhifadhi Quran ambayo ina manufaa kwao badala ya kutumia muda mwingi katika mambo yasiyo kuwa na faida kwa nchi.

"Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikishirikiana nasisi kwenye mambo mengi ikiwemo ya kidini siyo yale ya kidemokrasia peke yake, hivyo tutumie fursa hii kujifunza na kuyafanyia kai yale wanayotufundisha", alisema Sheikh Salum.

Said ambaye ni moja kati ya vijana wanaokwenda nchini humo, alisema matarajio yao makumbwa ni kushiriki mashindano hayo kikamilifu na kurudi na ushindi.

Aliwataka washiriki walioshindwa kupatana nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo kutokata tamaa na kujiandaa kwa ajili ya mashindano ya mwakani.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.