Taarifa zilizotufikia hivi sasa tupo hapa Maisara ni kwamba tayari miili mitatu imeopolewa hivi asubuhi na hivyo kufikisha idadi ya waliofariki kufikia 33.
Jitihada zinaendelea kutafuta waliobakia. Meli ilikuwa na abiria 248 na wafanyakazi tisa kwa mujibu wa Manifesto ingawa maelezo ya wasafiri walionusurika wanasema idadi hiyo ni ndogo.
Raia mmoja wa kigeni ambaye bado hajatambulika utaifa wake pia ni miongoni mwa waliofariki katika ajali hii.
Asantee sana tu kwa Update ingawaa Idadi inaonekana kua badoo haijatuliaa kila mtu anasema tofauti...? Ishallah mola atawasaidia wote Amein
ReplyDelete