Habari za Punde

Miili 12 yazikwa ufukweni kisiwani Bawe

Hafsa Golo na Madina Issa
MAITI 12 zinazoaminika zimetokana na ajali ya MV. Skagit zilizookotwa katika kisiwa cha Bawe, zimelazimika kuzikwa ufukweni mwa kisiwa hicho kutokana na kuharibika sana.

Akizungumza na waandishi wa habari hizi, mmoja kati ya waokoaji Khalid Said Suleiman alisema wamelazimika kuzizika maiti hizo kutokana kuwa katika hali mbaya na kuzisafirisha masafa marefu zinaweza kuleta athari za kiafya kwa waokoaji.

Alisema wangeweza kuzilta hadi katika kisiwa cha Unguja, lakini changamoto ya vifaa ubebaji wa maiti hizo nalo ni miongoni mwa tatizo linaloathiri zoezi la uokoaji.

Alisema pamoja na kuendelea kwa zoezi hilo kumekuwa na changamoto mbali mbali ambazo zimewapelekea kufanya kazi katika mazingira magumu huku wakijikuta wananjimwa misaada wa mashirikiano.

“Miili imeharibika sana hatunabudi kuwazika pembezoni mwa bahari kwani zimeharibika kiasi kwamba nyngine hazina viungo kamili”,alisema.

Alisema mbali na kujitolea lakini zoezi hilo lilifanyika katika mazingira magumu kiasi ambacho kimewasababishia kupata changamoto mbalimbali katika utendaji wao wa kazi huku wakivumilia mazito na kujali zaidi uzalendo na kujenga hisia za ubinaadamu.

Hata hivyo ameiyomba serikali kutafuata vyombo vya kisasa ili litakapotokezea tatizo waweze kuwarahisishia waokozi kufanya kazi kwa ufanisi na kwa wakati muafaka.

Alisema ni muhimu bandari ikawa na kifaa cha Eco Soundes Scannes, na Fish Firdes ambazo zinauwezo wa kusoma na kugundua kitu cha chuma ambacho kipo chini ya bahari (DETECT).

Sambamba na hayo alisikitishwa na kitendo cha serikali cha kutopokea ushauri wa awali waliopewa na waokozi wazalendo wa kukimbilia haraka katika tukio hali ambayo ingewezekana kujulikana meli hiyo ipo sehemu gani

Kwa upande wa waokozi kutoka kikosi cha msalaba mwekundu, pamoja na jumuiya ya maendeleo ya wavuvi Kojani (kofdo), walisema pamoja na kufanya kazi hiyo kwa moyo na uzalendo wa nchi yao lakini wamesikitishwa na usimamizi mbovu wa kamati ya maafa kwani imewapa wakati mgumu katika kufuatilia uokozi wa miili ya marehemu hao.

Mmoja wa mwanachama wa msalaba mwakundu Shaban Juma Kambi alisema kuwa kutokana na hali ngumu ya upatikanaji wa vifaa na kuhofia usalama wa afya zao jana walitishia kutoendelea na zoezi hilo.

Nae muokozi wa Kojani omar Kombo Omar ameiomba Serikali wakati litapomalizika zoezi hilo ni vyema kuwapeleka katika uchunguzi wa afya zao ili waweze kupata matibabu mapema ikiwa wamekumbwa na tatizo la kiafya.

2 comments:

  1. Nduguzangu endeleeni na uzalendo inshaallah allah ndie mlipaji msiitegemee hata kidogo nchi na serikali ya muungano.

    ReplyDelete
  2. Hizi kero za muungano sasa naona imekua bangi!...hata mtu akigombana na mke wake nyumbani anaweza kusema ni matataizo ya muungano!

    Haya mambo ya uokoaji ktk hatua hii ni mambo ya yetu na serikali yetu ya mapinduzi ya Z'bar...hapa muungano hauhusiki!

    Ndugu zangu tukumbuke, kama vile tunavyodai baadhi ya mambo yatoke kwenye muungano ili yawe chini ya SMZ ndivyo vivyo wajibu wa kutatua matatizo yakitokea unavyokua kwa serikali yetu!...tusilalamikia wengine watatusaidia tu pale watapopenda na watapokua na uwezo!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.