Habari za Punde

Salamu za Rambirambi kutoka Chuma Blogs





CHUMA BLOGS imepokea kwa masikitiko taarifa za kuzama kwa Meli ya MV Skagit jana eneo la Chumbe jirani na Bandari ya Zanzibar. 
Meli hiyo iliyokuwa na watu wanaokadiriwa kuwa 290 ilizama wakati ikitokea Dar es Salaam kuelekea Unguja, Zanzibar. Maiti zaidi ya 30 mpaka sasa zimeokolewa kutoka baharini na zoezi la uokoaji linaendelea.
Tunaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na tukio hili.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi. 

INNA LILLAH WA INNA ILLAYH RAJIUUN. 



Imetolewa na
SALIM CHUMA

JULAI 20, 2012

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.