Habari za Punde

WAZIRI wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Zainab Omar Mohammed amesema wizara yake ina mashirikiano mazuri na Wizara za Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika pamoja na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko katika masuala ya ushirika wa Wajasiamali wa Zanzibar hasa katika maonesho ya biashara ya Kimataifa ya Sabasaba na ya Afrika Mashariki.

Waziri Zainab aliyasema hayo huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi linaloendelea na vikao vyake Chukwani nje kodogo ya mji wa Zanmzibar, wakati akijibu suala la mwalikishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub lililohoji kwanini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haiweki chombo kimoja cha kusaidia wajasiriamali Zanzibar, badala ya kazi hiyo kufanya na Wizara zaid ya moja.

Waziri huyo alisema mashirikiano hayo pia yalilenga katika masuala ya Ushirika wa Wajasiriamali wa Zanzibar katika soko la Jumapili ikiwa ni pamoja na namna ya kuongeza ubora wa bidhaa zinazozalishwa.

Aidha aliongeza kuwa mashirikiano katika njia za kuimarisha vikundi vya ujasiriamali ikiwemo namna ya kuwapatia mikopo na mafunzo wajasiriamali hao.

Waziri Zainab alisema katika kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wake, hakuna ubaya kwa Wizara yake kushirikiana na vyombo vingi vyenye lengo sawa la kumuendeleza mjasiriamali.

Akieleza hayo kufuatia swali lililoulizwa na Mwakili wa Muyuni Jaku Hashim nAyoub alietakam kujua suala la kuhamasisha wajasiriamali kuzalisha zaidi mazao ya mdalasizi pamoja na hiliki, Waziri Zainab alisema mpango wa kuhamasisha Wajasiriamali katika wizara yake upo kupitia ushiriki wao hasa katika maonesho ya biashara yanayowahamasisha wajasiriamali hao katika kupata uelewa ikiwa pamoja na mialiko zaidi juu masoko ya Zanzibar na nje ya Zanzibar.



Wizara Kuifanyia Matengenezo Skuli ya Migombani.

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali inakusudia kuifanyia matengenezo Skuli ya Msingi Migombani kutokana na hali ya uchakavu wa skuli hiyo.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo Zahra Ali Hamad alisema skuli ya Migombani ni miongoni mwa skuli kongwe ambazo zinahitaji matengenezo ya mara kwa mara ili kurudisha uimara wa skuli hiyo.

Akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mohammed Said Mohammed alietaka kujua Serikali inampango gani wa kuyafanyia matengenezo majengo ya Skuli ya Mogombani kukokana na uchakavu wake.

Naibu waziri huyo alisema Wiraza yake inampango wa kukarabati majengo pamoja na kutia madirisha kwa usalama wa mali za skuli hiyo.

Aliongeza kuwa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012-2013 inalenga kuifanyia matengenezo makubwa skuli endapo uwezo wa fedha ukiruhusu

Akizungumzia suala la kupatiwa madirisha kwa skuli hiyo kufuatia swali lililoulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Mpendae lililouliza ni lini skuli hiyo itapatiwa madirisha ili wananchi warudishe imani yao.

Waziri Zahra alikiri kuwepo kwa tatizo hilo nakusema kuwa miongoni mwa matengenezo yaliyofanywa katika skuli huyo ni pamoja na kusawazisha kuvuja katika mabanda yote ya skuli kwa kuezeka majengo hayo, sambamba na kujenga vyoo.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.