Habari za Punde

Sakata la Mgao wa Fedha za zawadi - ZFA yasimamisha wachezaji wa Zanzibar Heroes

Chama cha soka Zanzibar kimewasimamisha wachezaji 16 wa Zanzibar heroes.

Rais wa ZFA Amani Ibrahim Makungu alisema uamuzi huu una lengo la kurudisha nidhamu katika timu hiyo ya taifa baada ya wacheza kujiamulia wenyewe kugawana pesa za zawadi ya Dola 10000 walizpzipata kwa kuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya Cecafa yaliyamalizika karibuni.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, iliyoshiriki michuano ya Chalenji iliyofikia tamati Desemba 8, mjini Kampala, Uganda, wameeleza sababu ya kugawana wenyewe fedha ya zawadi ya mshindi wa tatu, wamefanya hivyo kwa kutambua kuwa wasingeambulia kitu kama wangesubiri kugawiwa na viongozi.


“Yaweza kuwa si utaratibu mzuri wa kuamua kujigawia fedha za zawadi, lakini tumefanya hivi tukiamini wazi kuwa kama zingefika mikononi mwa viongozi, fedha hizi zisingetufikia,” alisema mmoja wa wachezaji na kuongeza: “ZFA wasingetupatia pesa hizi. Sasa kwa kulitambua hilo baada ya kujeruhiwa mara kadhaa huko nyuma kwenye mashindano mengine tukaamua kugawana.
 
Rais Makungu amesema uamuzi hua wa kuwafungia umekuja baada ya wachezaji ao kutakiwa kurudisha fedha hizo na ni wachezaji wane tu waliorudisha kati ya 20.
 
Makungu alisema kutokana na uamuzi huo wachezaji wote walioteuliwa timu ya Taifa ya Tanzania na ambao hawajarudisha pesa itabidi waondolewe katika timu hiyo na tayari ZFA imeshawajuulisha TFF.
 
Uamuzi huo utaweza kuwaathiri wachezaji sita kutoka Zanzibar walio katika timu ya Taifa nao ni Aggery Morris, Samir Nuhu, Mwadini Ally, Nadir Haroub, Nassor Masoud na Khamis Mcha

2 comments:

  1. ZFA watumie busara ktk kutatua sakata hili kwani linaonekana kuwa na athari kwa pande zote zinazohusika.

    Kuwafungia wachezaji kutainyima Z'bar uwakilishi ktk timu ya taifa na kuathiri ajira za vijana wetu.

    Hata hivyo na kuwaachia vijana kuchukua uwamuzi wa namna hii kutaathiri sana nidhamu zao na kuivunja moyo ZFA mabayo imejitahidi kiwezesha timu hapo ilipofika.

    ReplyDelete
  2. Nani atakae weza kuchukua busara simuoni hata mmoja kwasababu viongozi wingi wa ZFA wako kimaslahi, hivto vijipesa walivyopata timu ya Zanzibar ndio wanavyovipigia macho wapate kwenda kununuwa kitoweo...japo kuwa si vizuri ya wachezaji walivyofanya, ila kunatakiwa kutumike hekma ili kuwe na makubaliano kwa pande zote mbili...mie kwa hesabu zangu za haraka haraka kuna wachezaji si kama wana shida nazo kwasababu ni pesa ndogo ukiangalia dolla elfu kumi kwa watu zaidi ya 20 basi wamepata kila mchezaji dolla 400 ambazo si kitu kwao ila ni kuonyesha jamii kuwa washachoka kudhulimiwa kama wanavyosema

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.