Habari za Punde

Tahadhari ya mvua kubwa na upepo kutoka mamlaka ya hali ya hewa

Taarifa kwa umma

Mvua kubwa, Upepo Mkali na Mawimbi makubwa kwa maeneo ya Pwani Taarifa Na.
20130101-01
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 7:30 Mchana
Daraja la Taarifa:
1:Taarifa 2:Ushauri 3:Tahadhari
4:Tahadhari Kubwa:
Ushauri
Kuanzia:
Tarehe
02 Januari, 2013
Mpaka:
Tarehe
03 Januari, 2013
Aina ya Tukio Linalotarjiwa
Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku ), upepo mkali unaozidi km 40 kwa saa na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2 (maeneo ya Pwani)
Kiwango cha uhakika:
Wastani
Maeneo yatakayoadhirika
Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Lindi na Mtwara
Maelezo:
Kuwepo kwa kimbunga “DUMILE” kaskazini-mashariki mwa Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo ya kusini mwa Tanzania
Angalizo:
Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu wanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.