Habari za Punde

Waliokufa ajali ya boti Ziwa Tanganyika watambuliwa


Na Mwandishi wetu
IMETHIBITIKA kuwa watu 9 wamefariki dunia na wengine 12 hawajulikani waliko baada ya boti ya abiria kuzama katika Ziwa Tanganyika nchini Tanzania.

Taarifa zinasema kuwa, boti hiyo ilizama baada ya kukumbwa na dhuruba ambapo watu wengine 64 wameokolewa.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kigoma, Fraiser Kashai amethibitisha hayo na kusema kuwa boti hiyo inayoitwa 'Tunusuru Yarabi' ilikuwa ikitokea Kirando mkoani Rukwa ikielekea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Rumonge Burundi na ilikuwa imebeba abiria, shehena ya dagaa, vyakula na bidhaa za viwandani.


Baadhi ya abiria walionusurika waliokuwa wakisafiri na boti hiyo wamesema, pamoja na kuwa dhuruba ndiyo iliyosababisha ajali hiyo lakini shehena kubwa ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vimebebebwa vilichangia kuzama boti hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.