MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Zanzibar (ZAWA) Mustafa Ali Garu, akitiliana saini ya makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa Kisima kwa Ajili ya Jimbo la Kikwajuni na Mwakilishi wa NGos ya Tanzania Uth Icon, Katibu Mtendaji ya Ngos hiyo Abdalla Khamis Suleiman, makubaliano hayo yamefanyika katika Ofisi za ZAWA Mabluu jana,. Mradi huo utalinufaisha Jimbo hilo na kuondoa tatizo la maji, anayeshuhudia Mbunge wa Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Mustafa Ali Garu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo utakavyonufaisha Jimbo hilo na kupunguza kero ya maji na kusema Kisima hicho kitachimbwa kaburi kikombe na matanga yake yatawekwa Mnara wa Mbao ili kusambaza kaji hayo kwa jimbo la Kikwajuni.,kulia Mbunge wa Kikwajuni Hamadi Masauni na Meya wa Mji wa Zanzibar na Diwani wa Kilimani Khatib Abrahaman.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni akizungumza baada ya utiaji wa saini ya Mradi Mkubwa wa kusambaza maji katika Jimbo lake uliofadhiliwa na Ngos ya TA, Mradi huo utakuwa na awamu mbili ya kwanza kuchimba kisima na awamu ya pili ujenzi wa tanki la maji.
Waheshimiwa Madiwani wa Jimbo la Kikwajuni wakishughudia utiaji wa saini ya Mradi Mkubwa wa Maji katika Jimbo lao.
No comments:
Post a Comment