Habari za Punde

Bonanza la Soko Supa Chini ya Udhamini wa Zantel.

Mchezaji wa timu ya makontena michezani akiokoa mpira katika mchezo wa Supa Soka unaofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja,hufanyika wakati wa usiku, timu ya makontena michezani imeshinda 1--0.
Golikipa wa timu ya Makontena Michezani akiokoa mpira golini kwake na huku mchezaji wa timu ya Turky, akijaribu kuuzuia mpira huo ikiwa ni mchezo wa Bonaza la Supa Soka linalofanyika katika uwanja wa timu ya malindi mnazi mmoja, timu ya Kontena Michezani imeshinda kwa 1--0.
Kizaaza katika goli la timu ya makontena michezani
Wachezaji wa timu ya makontena michezani wakiwa katika mapumziko wakipata maelekezo kutoka kwa kiongozi wa timu hiyo.ikiwa imeshashinda bao 1--0.
Wachezaji wa timu ya Turky wakiwa mapumziko baada kurowa kwa bao moja dhidi ya timu ya makontena michezani.
Golikia wa timu ya Turky akidaka mpira. na huku mchezaji wa timu ya makontena michezani akiwa karibu na kusubiri 


Mchezaji wa timu ya Zantel akiwapita wachezaji wa timu ya Appole katika michezo maalum ya Bonaza la Supa Soka lililodhaminiwa na Kampuni ya Zatel , hufanyika wakati wa usiku, timu hizo zimetoka sare ya 1--1. 

Mchezaji wa timu ya Appole akiwa na mpira akijaribu kumpita mchezaji wa timu ya Zantel katika mchezo wa Bonaza la Supa Soka linaloshirikisha timu 12, katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 1--1.
Viongozi wa timun ya Zantel wakifuatilia mchezo wa timu yao na Apppole, mchezo huo umetoka sare ya 1--1. 
Mchezaji wa timu ya Veterani ya KMKM akizuiya mpira na huku beki wa timu ya PBZ akijaribu kumzuia katika mchezo huo wa Bonaza la Supa Soka linalofanyika katika viwanja vya malindi mnazi mmoja, timu hizo zimetoka sare ya 1--1.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.