Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein Ajumuika na Wananchi wa Wilaya ya Wete katika Futari Ikulu Wete.



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakisalimiana na Wanancni waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa karume Pemba jana,Rais yupo kisiwani humo ajili ya kuwafutarisha Wananchi,ikiwa ni kawaida yake kila ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhan

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alijumuika na Waislamu na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika Swala ya Magharibi kabla ya kufutari nao pamoja kwa futari aliyowaandalia wananchi hao jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Wananchi na waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba waiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi,baada ya Swala ya Magharibi,na kuendelea na Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Wete


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto)alipojumuika na Viongozi na wananchi wa na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika
futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba


 Wananchi wa Mkoa wa Kasakazini Pemba walipojumuika kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba


 Akina Mama wa Mkoa wa Kaskazini Pemba walihudhuria katika futari walioyoalikwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama mwanamwema Shein,jana katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba


 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi,akitoa shukurani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa Wananchi waliohudhuria katika chakula cha futari alichowaandalia Wananchi hao jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Wananchi baada ya kufutari nao kwa pamoja jana katika futari aliyowaalika katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

1 comment:

  1. Siku ya malipo kuna kazi kweli, katika mwezi huu mtukufu munashiriki katika futari na familia zenu wakati baadhi ya mashekhe wamewekwa ndani pasi haki kwa malengo ya kisiasa halafu mtu ategemee pepo, kweli hili linawezekana? Ikiwa siku hiyo kila mja atalipwa hata kama ni kiwango cha DHARRAT, ni lazima tutafakari hii dunia ni ya kupita tu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.