Habari za Punde

Jengo la Historia la Livingstone Zenj

Jengo la historia katika kisiwa cha Zanzibar ni la Livingstone lilioko katika maeneo ya kinazini Unguja na lilikuwa likitowa huduma ya Ofisi ya Utalii Zanzibar kabla ya Idara hiyo kuvunjwa, na hutembelewa na Wageni wanaofika Zanzibar kutembelea sehemu mbalimbali za historia katika visiwa vya Unguja.kwa sasa linatumiwa na jumuiya ya wafanyabiashara Zanzibar,  

3 comments:

  1. ilikuwa ni mahali pa kupeleka watalii ,vipi lile jumba la machinjioni bado lipo lililokuwa pembeni yake ?

    ReplyDelete
  2. Ni kweli hili jengo ni la kihistoria. Naomba kusahihisha sarufi kidogo. Mkuu, ulipaswa uandike "Jengo la historia katika kisiwa cha Zanzibar ni la Livingstone lililoko na sio lilioko".Hivyo ndivyo ngeli zitakavyokubaliana. Shukran.

    ReplyDelete
  3. Sijui ni lini picha hii imepigwa, lkn. mara ya mwisho kulitembelea jengo hili tarehe 13/11/2013 lilikua ktk hali mabaya kimandhari.

    Kama sehemu ya 'hobby' yangu tokea nikiwa mw'funzi hupenda kutembelea majengo ya historia mara kwa mara.

    Likizo yangu ya mwaka huu, nilitembelea 'Living stone house', Z'bar high court building na nilifarijika kuliona likiwa ktk ukarabati, Beti la jaibu ambalo nililiona ktk Blog hii, ikiwa sehemu yake moja imeporomoka bila ya matengenezo huku WAHADIMU wakihangaika kujenga mnara wa kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi!

    Binafsi siamini kama mnara huo utavutia watalii kama inavyodaiwa ila ni miongoni mwa njia za kuhalalisha (ku'jusify') ulaji fedha.

    Nilikua na matumaini makubwa na mabadiliko mbali mbali ya uongozi na wimbi la vijana wetu wanaopata elimu ya juu hapo Z'bar ktk kubadili hali ya mambo lkn. sasa matumaini yamekwisha!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.