Habari za Punde

Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Zanzibar Yasoma Maulid ya Mtume SAW

Mgeni rasmin katika maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW, Mhe. Fatma Ferej akijumuika katika maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW yalioandaliwa na Jumiya ya Wanawake wa Kiislam  Zanzibar, yaliofanyika katika viwanja vya Masjid Mushawar Muembesauri Zanzibar. 
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiungana na Waislam wengine Duniani kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S A W, yaliofanyika katika viwanja vya Masjid Mushawar muembesauri Zanzibar na kuhudhuriwa na Waumini wa mji wa Unguja.m
Wanafunzi wa Madrasatul Mutabina Muembemakumbi wakisoma Qusda katika maulid hayo ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW.

Wanafunzi wa Madrasa wakionesho onesho jinsi ya maovu yanayofanywa na Watoto wasiokuwa na maadili na kuacha mufundisho ya wazazi wao.

Ulti Bi Saada akitowa mawaidha kuhusu upotofu wa Mawasiliano na mafanikio yake wakati wa matumizi yake kuna baadhi ya watu hutumia kinyume na matumiza yaliokusudiwa. Hutumia kwa kutuma mambo yasio kuwa na maadili ya Kiislam, kwa kutuma vitu vitu visivyo stahiki. Mwasiliano hayo yamesaidia kuwasiliana na Wazazi na jamaa walio mbali nawe lakini sivyo hivyo hutumika kwa mambo mengine.   
Wanafunzi wa Madrasatul Tabria ya Mombasa Unguja wakisoma Qasda 


Wanajumuiya wakisoma dua baada ya kumaliza kwa Maulid hayo ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW, yaliofanyika katika viwanja vya Masjid Mushawar muembeshauri Zanzibar.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.