Na Hafsa Golo
WANAFUNZI wa skuli mpya ya sekondari ya Mpendae
wamelazimika kukatisha baadhi ya vipindi vya masomo, baada ya zaidi ya
wanafunzi 10 kuchagawa jana.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:00 na saa
5:00 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Wanafunzi waliokutwa na mkasa huo ni wanawake
wanaosoma kidatu cha pili na nne, hali iliyosababisha taharuki kubwa na
kusababisha walimu kusitisha masomo.
Mwandishi wa habari hizo alipowasili skuli hapo
alishuhudia makundi ya wanafunzi wakikimbia ovyo wengine wakirejea nyumbani.
Mwanafunzi mmoja wa kidatu cha nne, Subira Mgeni
aliliambia gazeti hili kwamba tukio hilo limewaweka katika wakati mgumu na
kusababisha kukosa vipindi muhimu.
Mwalimu Salim Mohammed Khamis, alisema chanzo cha
tukio hilo ni kuwepo mazingira ya kishirikina huku baadhi ya wanafunzi kukiuka
taratibu za misingi ya dini na hatimae wadudu waovu huwasumbua.
Alisema ni vyema wazazi kuwa makini juu ya uangalizi
wa watoto wao wanapokwenda skuli kwa kuhakikisha wanafuata maadili na wanaepuka
kutumia vifaa visivyostahiki ikiwemo kujitia manukato.
Kuchagawa??? kwanini iwe kwa wanafunzi wa kike tu, kulikoni !!
ReplyDelete