Habari za Punde

Habari Zisizokuwa za Ukweli Zilizoenezwa Zanzibar kwa Njia ya SMS Sio za Kweli kuhusiana na Mwalim Haroun

Kwa mujibu wa Ndugu wa Karibu wa Mhe. Haroun Ali Suleiman, wamekanusha taarifa zilizosambazwa kwa Wananchi wa Zanzibar kwa amefaridi dunia,Habari hizo sio kwele kwa na Jamaa na Ndugu wa Mhe Haroun wamekanusha habari hiyo kuwa ni uzushi, uliovumishwa na Watu wasiojulikana 

Mmoja wa wana Familia amesama Ndugu yao Mwalim Haroun  anaendelea vizuri na matibabu na hali yake inaendelea vizuri na kuzidi kuimarika .Mwalim Haroun amepelekwa Nchi Afrika Kusini kupata matibabu ya maradhi ya moyo. Na kwa sasa hali yake iko nzuri akiendelea na Matibabu yake katika hospitali  Nchini Afrika Kusini. 

Uvumi huu ulizagaa leo katika majira ya mchana kupitia njia ya SMS  na kusambazwa kwa watu mbalimbali katika visiwa vya Zanzibar na vitongoji vyake na watu wengi wameshtushwa na taarifa hiyo isio kuwa na ukweli ndani yake 

Wamesema Ndugu yao yuko Salama na anaendelea na matibabu yake. nchini Afrika Kusini.
  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.