Habari za Punde

Prof. Dkt Monzer Kahf, azungumza na Waandishi wa Habari faida za Benki ya Kiislam kwa Wananchi na Nchi.

Profesa Dkt. Monzer Kahf, akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na Benki ya Kiislam zinavyoedeshwa na faida zinazopatikana kwa Nchi na Wananchi.kwa kutumia Benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya Watu wa Zanzibar Mhe. Juma Amour, akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya PBZ Islamic jengo la Bima Mpirani Zanzibar.

Prof. Dkt. Monzer Kahf, akizungumza mafanikio ya Benki za Kiislam Duniani zinavyoinua Uchumi wa Wananchi na Nchi kwa kuazishwa kwake,na faida inayopatikana kupitia Benki hiyoakizungumza  na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar kuelezea umuhimu wa kuazishwa kwake na matumizi ya Benki hizo.kwa sasa tayari zaidi ya Benki za Kiislam 600 tayari zimeazishwa katika nchi mbalimbali Duniani. 
Prof. Dkt Monzer Kahaf, akisisitiza jambo wakati akijibu suali aliloulizwa kuhusiana na benki ya Kiislam, kuazishwa kwake si inaowa benki za kawaidi na kutowa mfano PBZ, ikiwa na Benki ya kawaida na  ya Kiislam.  
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ltd. Mhe Juma Amour akijibu suali ya kuhusiana na Benki ya Kawaida na ya Kiislam, juu ya moja inaweza kuanguka katika haduma zake za Kibenki, na kujibu Benki ya Kiislam imepata wateja wengi na kuingiza faida kubwa katika kipindi kidogo na wateja wengi ni kutoka benki ya PBZ ya kawaidi huamia Islamic PBZ, Hakuta tatizo la aina yoyote kibenki bali kila siku kiwango cha PBZ kinazidi kukuwa.Kupitia Islamic PBZ. 


Shekh. Jabir, akitowa ufafanizi wa Benki za Kiislam jinsi ya huduma zake zilizo bora na kuvutia wateja.

Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Prof. Dkt Monzer, katika ukumbi wa mkutano wa Makao Makuu ya PBZ Islamic, Mpirani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.