Habari za Punde

Bingwa mtetezi na Makamu wake watupwa nje Kipwida Cup

 Kiungo wa maskani ya Miembeni Omar Tamim ‘Omirey’ mwenye jezi ya njano akiwania mpira mbele ya mlinzi wa TRA Moh’d Hassan.
 Mlinzi wa timu ya TRA Haji Abdi akiokoa mpira uliomtoka mshambuliaji wa maskani ya Miembeni Juma Moh’d Philipo kwenye pambano la robo fainali ya tatu ya mashindano ya Kipwida Cup huko Maungani.
  Daktari wa vijana wa Miembeni Habibu Mfaume na shabiki wa timu hiyo Kusila wakimtoa nje mchezaji Amour Janja baada ya kupata dhoruba kutoka kwa beki wa TRA .

Mashabiki wa maskani ya Miembeni wakishangilia bao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji Juma Moh’d Philipo. Hata hivyo pambano hilo lilimazika kwa TRA kutoka na ushindi wa mabao 6-5 dhidi ya Miembeni. (Picha zote na Ali Cheupe)

Na Ali Cheupe
Timu ya TRA wamefanikiwa kuwaondosha kwenye mashindano ya Kipwida Cup yanayoendelea huko Maungani vijana wa Maskani ya Miembeni baada ya kuifunga mabao 6-5 kwenye pambano la robo fainali ya tatu hapo jana.

Miembeni ambao walikuwa makamu bingwa wa mashindano hayo walilazimika kwenda mapunziko huku kukiwa hakuna mbabe.

Kipindi cha pili kilianza kwa TRA kulishambulia lango la wapinzani wao na dakika ya 54 mshambuliaji Abrahman Othman aliweza kuipatia timu yake bao la kuongoza.

Kuingia kwa bao hilo kuliwafanya viongozi wa Miembeni kusimama na kutoa maelekezo kwa wachezaji wao na dakika ya 63 ilitosha kwa mchezaji Rashid Abdalla ‘Karihe mdogo’ kuweka majaro safi langoni mwa TRA na mshambuliaji Juma Mph’d Philipo hakufanya ajizi kwa kuukwamisha mpira wavuni na kusawazisha bao hilo.

Mara baada ya dakika 90 kumalizika huku matokeo yakiwa sare ya bao moja kwa moja sheria ya mikwaju ya penalty ilifuata ili kuweza kupata mshindi.

Katika mchakato huo TRA waliweza kuwatupa nje Maskani ya Miembeni kwa penalty 5-4.
Penati za TRA zilifungwa na Haji Ramadhan Mwambe, Suleiman Ali Senga, Ame Machano, Juma Kukuti na Abrahman Othman. Kwa upande wa Miembeni zilifungwa na Kaptein Kibata, Ahmed Malik, Amour Janja, Omar Tamim huku penalty ya Salum Seif ikitoka nje ya lango.

Leo hii kutafanyika pambano la robo fainali ya mwisho kati ya timu ya Machatu na mahasimu wao Mchawi hana rangi zote zikitokea sokoni Mwanakwerekwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.