Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Kupitisha Bajeti ya Wizara ya Afya Zanzibar.

Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Ali Abdalla akifuatilia michango ya kupitisha Vifungu vya Matumizi vyaWizara yaAfyaZanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Juma Duni akijibu swali la kituo cha afya katika mji mkongwe na kuonesha michoro ya ramani ya ujenzi wa kituo cha afya baada ya mazungumzona mamlaka ya mji mkongwe, kwa ujenzi wa kituo hicho na kujibu watakifanyia matengonezo kituo cha afya cha zamani kilichokuwa kikitowa huduma ya maklaria mkunazini.  
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura akichangia katika kupitisha vifungu vya matumizi vya Idara za Wizara ya Afya Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Ayoub akichangia kutaka kupata kauli ya Waziri tatizo la hospitali ya kidongochekundu kukosa umeme kwa deni lake kutokulipwa hadi sasa na majengo hayo kuwa katika hali ya kukosa huduma hiyo, alitaka kauli ya waziri tatizo hilolitamalizika lini.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar Mhe. Ismail Jussa akitaka majibu ya Kituo cha Afya katika mji mkongwe, baada ya hospitali ya Mnazimmoja kuwa ya Rufaa na Wananchi kupata huduma katika Vituo vya hospitali za Rahaleo, Mpendae,Kwamtipura, inabidi Wananchi wa Mji Mkongwe kupata huduma hiyo katika vituo hivyo.

Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini Mhe Mlinde akifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Juma Duni, akijibu hoja za kuzuiya Vifungu vya Matumizi vya Wizara hiyo, vilivyozuiliwa na Wajumbe kutaka majibu kutokana na vifungu hivyo.  
Waheshimiwa Mawaziri wakifuatilia michango ya Wajumbe wakati wa kupitisha Bajeti ya Wizara ya Afya Zanzibar. 
Waheshimiwa Wawakilishi wakimsikiliza Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Juma Duni, akijibu hoja za Wajumbe baada ya kuzuiya Vifungu vya Bajeti ili kupata majibu ya matumizi ya Vifungu hivyo.  
   Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakipitisha Vifungu vya Matumizi vya Wizara ya Afya Zanzibar
Mhe Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni akitoka ukumbi wa Baraza la Wawakilishi baada ya kupitishwa Bajeti yake na Wajumbe, akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar. Mhe Ismail Jussa wakitoka katika ukumbi mkutano.  
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Juma Duni, akizungumza na Watendaji wakuu wa Wizara yake baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara yake kupitishwa kwa mbindi na Wajumbe baada ya kurudishwa wiki iliyopita ili kufanyiwa marekebisho baadhi ya vifungu.     

1 comment:

  1. Haya na wewe Mr Juma Duni wafanyie tafrija ya kuipongeza wizara yako!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.