Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Kuchangia Bajeti ya Wizara ya Afya Leo.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Juma Duni akifuatilia michango ikiwasilishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakichangia Bajeti ya Wizara yake leo asubuhi.


Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakichangia Bajeti ya Wizara ya Afya Zanzibar.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Vitengo vyake wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wakichangia Bajeti yao leo asubuhi. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Ameir Kificho akitoka Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi baada ya kuahirishwa kwa Kikao cha Asubuhi kikijadili Bajeti ya Wizara ya Afya Zanzibar. 
Wanziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe, Dkt Mwinyihaji Mamake akitoka katika ukumbi wa mkutano wa Baraza la Wawakilishi baada ya kuahirishwa asubuhi leo.
Mwakilishi wa Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Waziri wa Habari Mhe. Said Ali Mbarouk, wakitika nje ya ukumbi wa Mkutano wa Baraza baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi kwa mapumziko mafupi ya mchana. 
Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni akitowa ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi.akiongozana na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni, akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya, baada ya Kikao cha asubuhi cha kuchangia Bajeti ya Afya na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi leo asubuhi.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.