Habari za Punde

Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China Chuo cha Habari Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio ChinaBi Xu Lin, akisalimiana na Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar kutembelea Darasa la Lugha ya China,linalotowa elimu hiyo katika Chuo hicho Vuga Zanzibar.  
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China Bi. Xu Lin, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Mwinyihaji Makame, alipofika kutembelea Darasa la Kichina katika Chuo hicho akiwakatika ziara yake Zanzibar.
Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar wakiwa darasani wakijifunza kuandika herufu za Kichina kutumia michoro ya karatasi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China Bi. Xu Lin, akizungumza na mmoja wa Mwanafunzi anayejifunza Kichina katika Chuo cha Uandishi wa Habari Vuga Zanzibar, alipofika Chuoni hapo kuangalia maendeleo yadarasa hilo.
Mkurugenzi wa Darasa la Kichina katika Chuo cha Uandishi wa Habari Vuga Ndg. Li Hong, akitowa maelezo ya maendeleo ya darasa hilo tangu kuazishwa kwa kutowa Elimu ya Lugha ya Kichina kwa Wanafunzi wa Chuo hicho na Waananchi wa Zanzibar kujifunza lugha hiyo.
      Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Vuga Zanzibar wakimsikiliza Bi Xu Lin akiwahutubia

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Mwinyihaji Makame, akihutubia wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China, Bi Xu Lin, alipofika kutembelea darasa la lugha ya Kichina  ( CONFUCIUS  - CRI Zanzibar ) 
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China Bi Xu Lin, akiwahutubia Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, alipofanya ziara ya kutembelea Chuo hicho na kuangalia maendeleo ya darasa hilo linalotowa mafunzo ya lugha ya kichana Zanzibar.
KAIMU Mkuu  wa Chuo cha Waandishi wa Habari Zanzibar Ndg. Rashid Omar, akimkabidhi picha ya sura yake Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China Bi Xu Lin, alipofika kutembelea Darasa la Lugha ya Kichina inayofundishwa katika Chuo hicho. 
NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha RedioChina, Ndg. Wang Minghua, akizungumza katika hafla hiyo ya kutembelea darasa la lugha ya Kichina katika Chuo cha Habari Zanzibar kuangalia maendeleo ya Mafunzo hayo. 


Mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari  Vuga Zanzibar Bi Asha Fum, akiimba wimbo maalum huimbwa wakati wa shughuli za harusi Nchini China, wakati wa hafla ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China, Bi. Xu Lin, alipofika kuoni hapo.na kupata fursa ya kwenda China kwa Mafunzo ya miaka mitatu. Kwa Ufadhili wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China.   
Bi Xu Ling akichukua picha ya Mwanafunzi Asha Fum, wakati akiimba wimbo wa Kichina katika hafla hiyo.




 Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Redio China Bi Xu Lin, akiwa na Ujumbe wake akionesha Gazeti la Shirika la Magazeti ya Serekali Zanzibar Zanzibar Leo, alipokuwa katika ziara yake kutembelea Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar.








No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.