Akinamama wa Makunduchi wakimsikiliza ndugu Mohamed Simba ambaye hayupo kwenye picha katika sherehe fupi ya utoaji wa simu.
Wanawake wa Makunduchi wapatiwa msaada wa simu ili kujiendeleza kiuchumi. Akitoa msaada huo kwa niaba ya Kamati ya wadi za Makunduchi, ndugu Mohamed Simba amewataka akinamama wa Kimakunduchi kutumia simu hizo kwa maendeleo. Wanawake waliopatiwa msaada huo ni wale walioshiriki kwenye mapishi ya chakula cha asili katika sherehe iliyofanyika skuli ya Kiongoni. Zaidi ya simu 200 zimetolewa.
No comments:
Post a Comment