Habari za Punde

Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL),Yachangia Shilingi Milioni 10 kwenye Mfuko wa IMETOSHA FOUNDATION

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.Kushoto ni Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi.
 Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani yatakayofanyika Machi 29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine pichani toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Jhiko Manyika “Jhikoman”.
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Picha na Othman Michuzi
……………………………………………
Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10 kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.
Akizunguma na waandishi wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu ni jukumu la kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania wameona umuhimu kuchangia harakati hizo,kwani hata sifa mbaya zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au kundi fulani. 
Amesema watu wengine wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya watu ambao wanaguswa na suala la mauji ya watu wenye ualbino.
Matembezi hayo yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe ambapo ujumbe wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za kukomesha mauaji ya watu hao wenye Ualbino.
Akizungumzia Matembezi hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema matembezi hayo hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki matembezi hayo.
mdimu amesema kuwa harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji ya watu wenye ualbino ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee kuwepo.
“Hatulengi masuala ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu wanaofanya hivyo washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia katika familia”amesma Mdimu.
Amesema harakati hizo zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao katika kuweza kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.