Habari za Punde

WATUMISHI KATIBA NA SHERIA WAMUAGA JOSEPH NDUNGURU ANAYESTAAFU LEO BAADA YA KUTIMIZA MIAKA 60

 Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60, akimlisha keki Katibu Muhtasi wake Bi. Fatuma Ngodoki jijini Dar es Salaam leo huku watumishi wengine wakishuhudia.
Mwanasheria katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Charles Mmbando akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika hiyo Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60.
Mhasibu katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Job Kiwory akimiminia kinywaji kisicho na kilevi Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara hiyo Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60. Kulia ni Mwanasheria katika Wizara hiyo Bw. Charles Mmbando.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph J.K. Ndunguru (mwenye tai) katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria jijini Dar es Salaam leo (Machi 20, 2015). Bw. Ndunguru anastaafu utumishi wa umma leo baada ya kutimiza miaka 60.
(Picha: Wizara ya Katiba na Sheria)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.