Habari za Punde

Mafunzo juu ya taratibu za uandikaji wa sheria na katiba yaliofanyika skuli ya Maandalizi Madungu Chake chake

 MRATIBU wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Fatma Hemed Khamis, akiwa makini kuwasilikiza wachangia ambao ni viongozi wa dini na kijamii, kwenye mafunzo yalioandaliwa na ZLSC juu ya taratibu za uandikaji wa sheria na katiba yaliofanyika skuli ya Maandalizi Madungu Chake chake, katika ni Afisa mipango wa kituo hicho Khalifan Amour Mohamed na kushoto ni mtoa mada Mohamed Ali Maalim, (picha na Haji Nassor, Pemba).
 WASHIRIKI ambao ni viongozi wa dini na kijamii wa mafunzo ya taratibu za uandikaji wa sheria na katiba yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar, tawi la Pemba na kufanyika skuli ya maandalizi Madungu Chakechake, (picha na Haji Nassor, Pemba
MSHIRIKI wa mafunzo ya taratibu za uandikaji wa katiba na sheria Hafidh Mohamed Salim kutoka Jumuia ya Maimamu Zanzibar JUMAZA, Pemba, akiuliza suali kwenye mafunzo yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar tawi la Pemba, na kufanyika skuli ya maandalizi Madungu Chake chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

MSHIRIKI wa mafunzo juu ya taratibu za uandikaji wa katiba na sheria Amini Haji Makame, akiuliza suali kwenye mafunzo yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar tawi la Pemba, na kufanyika skuli ya maandalizi Madungu Chake chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

Na Haji Nassor, Pemba
WANACHAMA  wa chama cha wafanyakazi wa huduma za  umma na afya ‘ZUPHE’ matawi ya Pemba, wamesema mafunzo ya sheria za kazi, yalioandaliwa na Kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC, hayakuwapa ufahamu pekee, bali kwao ni fursa ya kukutana na viongozi wao wakuu waliowatekeleza kwa muda mrefu.
Wanachama hao walisema tokea baadhi yao walipojiunga miaka zaidi ya minne iliopita na chama hicho, hawajawahi kukutana hata mara moja na uongozi wa juu wa chama, ambapo kupitia mafunzo hayo ndio wamewatambua.
Walisema mafunzo yalioandaliwa na ZLSC yamewasaidia kukutana na viongozi wao wakuu, akiwemo Katibu Mkuu na Katibu wa Kanda ya Pemba, jambo ambalo ni furasa adimu kwa vile viongozi hao wamekuwa wazito kupita kwenye matawi.
Hayo waliyasema jana kwenye mafunzo ya siku mbili yaliofanyika ofisi za ZLSC mjini Chake Chake, wakati walipokuwa wakichangia sheria kadhaa za kazi ikiwemo ile ya ajira no 11 ya mwaka 2005.

Wanachama hao walisema viongozi hao wamekuwa hawaonekani hata mara moja kwenye matawi, na wanacho ambulia wao ni mikato kupitia mishahar yao kwa ajili ya kukiendesha chama hicho, bila ya kupewa elimu na  chama  chao cha ZUPHE.
Sanura Salim kutoka wizara ya Afya, alisema amekuwa akikosa haki zake za likizo kutoka kwa mwajiri wake, ingawa kilio hicho hushindwa pakukipelekea kutokana na viongozi hao kutoonekana.
“Mimi nimeajiriwa tokea  waka 1985, na nimejiuga na  ZUPHE zamani, lakini nashindwa pakupeleka kilio changu simuoni katibu wa tawi, katibu Mkuu wala wa kanda, mimi nnachoambaulia ni mikato’’,alisema.
Nae Mohamed Hakim Ngawali alisema viongozi wa matawi ya ZUPHE, wamekuwa hawashughuliki na uwepo wa wanachama wao, ambapo baada ya kuwakampeni kuingia ndani ya chama hakuna jengine linaloendelea.
“Mimi niligonga gari wakati nikiwa kazini, basi nilishitakiwa na nawatafuta viongozi wa ‘ZUPHE’ alau nipate msaada siwaoni, ndio nawaona leo (jana) kwenye mafunzo haya’’,alifafanua.
Akijibu baadhi ya hoja hizo Katibu Mkuu wa ZUPHE, Jina Hassan Salima, alisema hata yeye anashangaa kuona viongozi wa matawi wanakaa muda mrefu bila ya kuwapitia wanachama.
“Mimi nashangaa kwamba viongozi wa matawi wanakaa muda mrefu bila ya kukutana na wanachama wetu, sasa hapa ufanisi utapatikana wapi, wakati kwenye mpango kazi wetu tunaweka kwamba kuwe na vikao’’,alifafanua.
 Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha huduma za sheria Zanzibar tawi la Pemba Fatma Hemed Khamis, aliwataka wanachama hao wasikae na kulalamika, juu ya ufahamu wa sheria za kazi ni vyema wakakitumia kituo hicho kwa kupata ushauri wa kisheria.
Fatma alisema kituo hicho pampoja na kazi nyengine, kipo kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi wanaodhani wameonewa au kuvunjiwa haki zao, ambapo kazi zote hizo zinafanywa kituoni hapo bila ya malipo.
“Jamani kwama viongozi wenu hamuwaoni kwenye matawi na mna mashaka ya kisheria njooni kituoni hapa, mtapata masada wa kisheria bure ili upata utaratibu wa kudai haki zako’’,alifafanua.
Akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa ZUPHE taifa, dk Zahran Mohamed Nassor, alisema suala la kujua sheria ni jukumu la kila mmoja na hasa kwa vile hakuna kinga kwa alietenda kosa kwa kinga ya kutokujua.
Akiwasilisha mada ya sheria ya ajira namba 11 ya mwaka 2005 mwanasheria wa serikali Mohamed Juma Ali, alisema sheria hiyo imepiga marufuku kudhalilishwa kwa mfanyakazi kwa nia ya kutaka kupandishwa cheo au jambo jengina linalofafanalo na hilo.

Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC, mada kadhaa zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na kanuni ya utumishi wa umma ya mwaka 2014, sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2011 na sheria ya mahusiano kazini ya mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.